FOREX NI NINI...?
Forex ni Kifupi cha Maneno Mawili.
1. Foreign
2. Exchange
Foreign + Exchange = For + Ex 👉FOREX.
Hii ni Biashara Ya Kuuza Na Kununua Sarafu Maarufu Duniani, mfano Dollar ya Marekani (USD), Dollar ya Canada (CAD), Japanese Yen (JPY) N.K
Biashara hii Ni Biashara Kubwa Zaid Duniani, Inayofanywa Kimataifa, Na Ina Mzunguuko Mkubwa Kuliko Biashara Yeyote ile Duniani. Kwa Siku Moja Mzunguuko wa Pesa Yake Ni Trilion Dollar 7 za Kimarekani (Huo Ni mzunguuko wa Siku Moja tu) Na Hakuna Soko lolote Linalofikia Kias hicho cha Pesa Zaid Ya Fx.
Kwa Miaka Ya Nyuma Forex ilkua Inafanywa Na Mabenk na Taasisi Kubwa Zenye Uwezo wa Kifedha Na Ilkua Ni Physical Business Kama Wafanyavyo Bureau De Change, ila Kutokana na Maendeleo ya Teknolojia, Wakaweka Mfumo Wa Online Trading Unaoruhusu Mtu Yeyote Kufanya Biashara Hata Ukiwa Na Mtaji wa Elfu 20 tu Za kitanzania Unaweza Kuifanya.
Soko la Fx.
Soko la Forex Lipo wazi Masaa 24 kwa Siku 5 za Wiki Yani Siku za Juma Unaweza Kufanya Kazi Muda Wowote Ule. Soko Hili Lipo Chini ya Uangalizi wa INTERNATIONAL MONETORY FUND (IMF) iliopo huko WashingTon DC. Kaz Ya IMF ni kuhakikisha Usawa Na Haki za Kila Mfanyabiashara.
Kwahio Soko la Fx ni 24/5 lipo Wazi, Na Ndio Soko Lenye Mzunguuko Mkubwa Wa Pesa Kwa Siku. Soko hili ni la Online Japo Japo Kituvo kipo Huko Marekan.
*What is Traded in Fx*
Kweny Fx kinachotradiwa ni Currencies.
Kumbukua Hii ni Biashara Ya Pesa Kwa Pesa. Mfano Nimeenda Bureau De Change Kupeleka Dollar ili wanipe TZS, Hii inamaanisha Kua Nmenunua TZS kwa Kutumia DOLLAR.
Biashara iliniitwe Biashara Ni lazima Kuwepo Na mabadilishano ya Kitu kwa Kitu, Mfano Ndio Huo Unaenda Benk na Dollar (Means unawapa dollar) ili wakupe TZS
Au Kwa Mfano wa Kawaida Kabsa Ni kwamba Unaenda Dukan na Elfu 3 ili wakupe Sukari yaani Nipe Nikupe.
Hivyo Kwenye Biashara ni lazmia Kuwe na Vitu Viwili kinachotolewa Na Kinachochukuliwa (Give and receive)
Safaru Zote Dunian Zina Herufi 3 Mfano TZS, KSH USD n.k
Mara Nying Heruf Mbili za Mwanzo Zinakua Ni Jina La Nchi kisha Heruf inayofata ni Jina La pesa inayotumika nchi Husika.
NB. Kwa Africa Ni nchi moja Tu yenye Sarafu yake Kwenye Soko la Forex Nchi hiyo Ni South Africa, Sarafu yao inaitwa *ZAR* (South African Rand)
Baadhi ya Sarafu na Majina Yao:
AUD 👉 Australian Dollar
USD 👉 United Stated Dollar
GBP 👉 Great British Pound
NZD 👉 New Zeland Dollar
CAD 👉 Canadian Dollar
JPY 👉 Japanese Yen
EUR 👉 Euro
N.k
Zipo Nying Utazijua Tu Zote
Market Participants
Kuna wahusika Wa 4:
1. Big Boys/Banks/Big institutions. Hawa Ndio Mabosi Wakubwa Waliowekeza Pesa Zao Kubwa Kwenye Hii Biashara. Mara Nying Hawa Hua Hawafanyi kaz Wao Wanawaajil Watu Ndio Waliendeshe Soko Watu Hawa Wanaitwa Market Makers.
2. Market Makers
Hawa Ni Wasomi Wanaotengeneza Fursa Za Soko Online Kupitia Charts 📈📉 Au Indicators za Kiuchumi, Kisiasa, hata Natural Disasters Pia, Mfano China Wapate Tetemeko la Ardhi Liue, Liharibu Mali na Miundo Mbinu Bas Lazima Uchumi Wapo Ushuke kwa Kias Fulan, Hivi vyote Wanavitoa Wao.
3. Brokers (Madalali)
Hawa Ndio Watu Wenye Mitaji ya Kati, Ukiwatoa Hao Bog Boys. Na Sisi Hua Tunajiunga Nao au Tunatrade Kupitia Migongo yao, Bila Hawa Madalali Sisi Wenye Mitaj midogo Tusingeweza Kufanya Hii Biashara. Hawa Ni kama Benki Ambazo Unasema Mimi Nitatrade Kupitia Benk/Dalali Flan Kule Utaonekana Wewe Innocent Sailen Unafanya Biashara Kupitia Dalali Fulan, na Yeye Kuna Kitu Anapata Sio Bure 😆😆. Ila Hua Ni kidogo Sanaaaaa Hawawez Kuchukua Hela Kubwa Maana Wakichukua Hela Kubwa Watu Wanawahama, Coz kuna Brokers Wengi Sana kwahio kila Mmoja Anajitahid Kujishusha ili Apate Watu Wengi, Mfano mm Hapo Kweny Hela Niliyoingiza Leo Laki 1.5 ya kwao ni Kama Shilingi Mia 5 tu 😆😆 Sema Wana watu Wengi Sanaaa ndo Mana Wanapata Faida.
4. Retail Traders/Wafanya Biashara Wa Leja leja 😆😆 Ndio Sisi Sasa, Wenye Mitaji ya Nyanya 😆😆🙌🙌 kwenye Rank Sisi Ndio Kundi la Mwisho ila Kuna Watu Wana Mitaji Mikubwa Sana unakuta Mtu ana Mtaji wa Trilion 1 ila Bado Wanamuita Mfanya Biashara Wa Leja Leja Maana Wao Wakubwa Wana Mizigo Sio Ya Mchezo 😆😆
The Concept Of Business
Biashara yoyote ile Unahusisha Vitu Viwili *Sell and Buy*
Siku Zote Una Sell kile Ambacho Hauna Umuhim Nacho Au Kisichokua Na Nguvu Kwako (Ndio Maana Unakiuza)
Uki-Buy, Unanunua Kile ambacho Kina Umuhim au Nguvu Kwako, Ndio maana Unakinunua.
Kwahio Unasell Kitu Dhaifu Kwako alaf Unabuy Kitu Chenye Thaman Kwako.
Kwenye Biashara Sell and Buy Hua ni Vitu Vinavyotokea Kwa Wakati Mmoja. When You Give (means You Sell), When You Receice Means You Buy.
Mfano.
Toa Elfu 1 Upate Ugali 😀 (Sell and Buy or Give and Receive)
Currency Pair
Pair hizi Zinakua Na Sarafu Mbili, mfano GBPJPY (GBP/JPY)
Sarafu ya Kwanza (Mkono wa Kulia) inaitwa *BASE CURRENCY*
Sarafu ya pili (Kushoto) inaitwa *QOUTE CURRENCY*
Mfamo.
AUDCAD 👉 Base ni *AUD* Qoute ni *CAD*
Market Order
Kwenye Software Tunazotumia Zina Ruhusu market Order Moja Tu, Yan Kama Ni Sell Unaweka Sell na Kama Ni Buy Unaweka Buy pekee, Hakuna Kusema Sell GBP, buy USD hapana, Tunasema SELL GBPUSD au Kama Ni buy Bas Utasema BUY GBPUSD
Market Order Hua Ni Kwaajili ya *Base* Currency, mfano Ukisema SELL GBPUSD (means Sell GBP, Buy USD) ila Hilo la Buy Hakitaonekana ila Wewe Unatakiwa Ujue hivyo kichwan.
Ukisema BUY GBPUSD, Means Buy GBP, sell USD.
Kwahio Market Order ni Moja Tu Kati ya Sell or Buy.
Ukisema Buy Means Base Currency ina Nguvu (Strong)Ndio Maana Una-ibuy
Ukisema Sell, Means Base Currency ni Weak ndio Maana UmeiSell.
Mfano, SELL GBPJPY 👉 Means GBP is Weak, JPY is Strong
BUY GBPJPY 👉 Means GBP Ni Strong, JPY ni Weak
UTAJUAJE SARAFU FULANI INA NGUVU KULIKO NYINGINE.
hapa Kuna Njia za Kufanya Uchambuzi wa SOKO.
1. Technical Analysis (Hii ndio Njia Ninayoona Ina nguvu kubwa sana.
2: Fundamental Analysis hii inahusu Uchambuz wa Factors Zinazoathiri Uchumi, Mfano Majanga ya Asili (Floods, EathQuek n.k), Siasa, Magonjwa Na vingine Vingi.
3. Sentimental Analysis (Hii inahusu Kuangalia Wenzako Wengi Wamesemaje Juu ya Pair Fulan Alaf unaangalia Wengi Waliko Unaungana Nao😆😆.
Zote Tutazisoma Kwa Undani.
Oky. Sasa Platform Inayotumika Kama Sehemu ya Kufanyia Biashara Inaitwa META TRADER (MT) inaweza Kua Version 4 (META TRADER 4) au Vesrion 5 (MT5)
ENTRY PRICE, TAKE PROFIT & STOP LOSS
Biashara Yoyote ile ina vitu hivyo Vi 3.
Entry Price (Thaman Ya Kuingilia Katika Biashara) mfano Umenunu Mahindi Debe 1 kwa Shiling 5000 ili ulifanyie Biashara (Uliuze), sasa Hio Bei uliyoingilia Kwenye Business ndio inaitwa Entry Price au Open Price
TAKE PROFIT
Ulinunua debe la mahind kwa 5000 ili Uliuze, sasa Utaamua Wewe Uliuze kwa Shiling Ngapi, Mfano Ukaamua Kuliuza Kwa 8000 basi hio Bei (8000) itakua ndio Take Profit
STOP LOSS
Ulinunua Kwa 5000 (Entry Price) ili ukaliuze ila Ulipofika Sokon Kwaajil ya Kuliuza Ukakuta Bei ya Kule Mbaya Zaid ya Ukiyonunulia Wewe, Sasa Unaamua Kuuza Kwa Hasara, Hasara Hii Kweny Fx Unaichagua Wewe Mwenyew Sio Mtu Mwingine, Iko Tofaut na Kweny Biashara za Kawaida Ambapo ikiamua Kukukata Inakukata Yote ila Kweny Fx unaamua Kiwango cha Hasara. Entry price ni 5000 unaweza Kuamua stop loss iwe 4500 yani upate Hasara
NB
soko likiwa Linapanda Juu BASE CURRENCY* Ni STRONG
likiwa Linashuka BASE CURRENCY Ni WEAK
Soko Linalopanda Linaitwa UPTREND MARKET
Soko Linaloshuka linaitwa DOWNTREND MARKET
Kila Candlestick Moja inaundwa Kwa muda Wake, Unaweza Kuamua Wewe Uweke Muda Gani, Unaweza Kuamua Kila Candleatick Moja Itengenezeke Baada Ya Dk 5. Huo Muda Ambao Candlestick Huundwa Unaitwa *TIME FRAME*
Je unawezazaje kutrade nakushughulika na mambo hayo yote? tusome kwanza kitu kiitwacho lot size
Tuna Aina 3 za Lot Size.
1. Mirco Lot Size
Inaanzia 0.01 Mpaka 0.09
0.01 ni Sawa Na 10Cent kwa Kila Pip 1.
So ikiwa 0.02 ni 20Cent kwa Pip 1
0.03 ni 30Cent Kwa kila Pip 1
N.k
KUMBUKA.
1USD = 100 Cent.
Swali.
1. Inno Alitrade GBPUSD akapata Pips 100, Alitumia Lot Size ya 0.01, Je Inno Alipata USD Ngapi?
2. Baraka Alitrade USDJPY, Alitumia Lot ya 0.03, Akatoka Na Pips 30. Je Baraka Alipata USD ngapi?
Aina Ya Pili ya Lot Size.
Mini Lot size
Hii inaanzia 0.1 mpaka 0.9 Ambapo 0.1 ni Sawa na USD 1 Kwa Pip 1.
Hizi Hazihitaj Calculations Za Cent maana Hazina Cent.
0.1 👉 USD 1 KWA PIP 1
Kwenye Soko Linaloshuka (Down Trend) Tunatakiwa Kusell. Hivyo Entry Price itakua Juu (Kubwa Kuliko Take Profit)
Mfano Umeingia Kweny 9.600 (Entry price), Tp yako inatakiwa Kua Ndogo Kwa Entry price Kwasababu Soko Linashuka Chini na Namba Zinapungua. Hivyo Tp Inaweza Kua 9.000 au Namba Yoyote ile Ndogo Kwa entry Price
Kwahio Kwenye Down Trend, Utapata Profit Kama Utasell, ila Ukibuy Ni Hasara.
Kwenye Uptrend Soko Linapanda Juu Hivyo Tunatakiwa Kubuy. Hapa Entry Price itakua Chini (Ndogo) ila Take Profit (Tp) itakua Kubwa. Mfano Entry Price 1.2000 alaf Tp Iwe 1.6000
Kwa Ufupi.
In Uptrend We Buy The Currency Pair.
SL itakua Ndogo Kwa Entry Price
TP itakua Kubwa kwa Entry Price.
In Down Trend We Sell tje Currency pair.
SL itakua Kubwa Kwa Entry Price
Tp itakua Ndogo kwa Entry Price.
Hizo Setting za SL na TP zitakusaidia Kujifunga Kwa Trade yako Automatic Hata Kama Hautakua Online itakuta Trade Imejifunga Eiza Kwa Kugusa SL au TP. Kwa Hio Ukiweka Trade Order yako Ukaseti Na Hizo TP na SL huna Shida Tena Na Hio Trade, Unafanya Mambo Yako Tu
KINACHOFUATA NI CANDLESTIC PARTTERN REFORMS AND ITS INFORMATION
..............................TUKUTANE PAET TWO...............................
Post a Comment