KEY LEVEL ( PURE PRICE ACTION ) PART FIVE

 Baada yakusoma pattern naomba tuangalie kitu kinachoitwa PURE PRICE ACTION

Tunapodeal na price action hapa huwa tunadeal na kitu kinachoitwa PPF (PAST, PRESENT AND FUTURE )

👉 *hapa huwa tunadeal na zone*

Ambazo hukaa katika mifumo miwili👇

👉 Zone zimegawanyika katika mifumo miwili ambayo ni;

👉 *vertical zones*

👉 *Horizontal zones*

Ambapo hapa hizo zone zinazoingia katika huo mfano ni hizi zifuatazo👇👇

👉 Resistance

👉 Control price

👉 Support


👉 Zone hizi hutumika kuyuonesha Soko wakati ULIOPITA, ULIOPO NA UJAO

👉 wakati uliopita na uliopo ndio unaotusaidia kupata mwelekeo wa Soko kwa wakati ujao


👉 Hapa huwa tunatumia Vitu vingi katika kuonesha hizi zones 

Moja wapo ni hizi zifuatazo;

1; horizontal trend line

2; Trendline za kawaida (unaweza kuipeleka uelekeo wowote)

3; mishale

4; njia ya maumbo yaweza kua mstatili ,mraba au pembe tatu

                                                        Tuanze na VERTICAL ZONES 


👉 Hizi ni zone zinazotumika kuonesha kingo ya market wakati inapanda au inashuka


Ndani yake tutaona  RESISTANCE ,CONTROL PRICE NA SUPPORT pamoja na kazi ya Kila Moja wapo👇


👉 Hapa tunaona hii chart Yetu ambapo Inatuonesha vertical zones na zikiwa zinaonesha charts ambayo ipo katika upward trend  mshale no 1 unaonesha resistance kitu ambacho dealers wakilifikisha zoko katika huo mwambao wanalirudisha lilikotoka ,hii inatuonesha tunaangalia wakati uliopita lilipita katika kingo ipi na hiyo RESISTANCE unapoichora unahakikisha kigo angalau Zaidi ya Mbili au Mbili zimegusa trendline yako hilo Eneo tuna liita SUPPLY ZONE  hapo deallers wanaweka order zao katika kusell , Mshale 2 unatuonesha CONTROL PRICE  hili Eneo ni mhimu sana kwaajili yakuweka TAKE PROFIT Mara nyingi dealers (market marker) wanatambua yakua wafanya Biashara huweka TAKE PROFIT zao katika kingo za mwisho yaani resistance na support na hivyo huamua kuligeuzia Soko katikati na traders wengi kujikuta TP zao hazijafikiwa hivyo hiyo sehem ya katikati ambapo dealers wanaishia wakati mwingine ndipo panapoitwa control price (mkondo wa chart) hapo ukiweka TP yako ni lazima TP yako ifikiwe na uchukue Faida Nje na hapo😆 kichapo




👉Tumalizie na mshale wa tatu katika hiyo chart


Huo mshale unatuonesha SUPPORT Eneo hili huwa linaitwa demand zone ambapo dealers huwa wanageuzazoko nakuanza kubuy 

👉unapochora mistali hii yote mitatu (zone hizi tatu) hakikisha unazicholea kwenye peaks za candlestick ambapo unahakikisha imeshika walau kingo Zaidi ya Mbili au mbili




Hizi ni chart inayotuonesha chart Yetu ikiwa katika downward trend

1👉 inatuonesha resistance (supply zone)Eneo la sellers kuingia sokoni

 2👉 Control price ( zone of Take profit)

3👉 support (Demand zone) Eneo la buyers kuingia sokoni


*Note usiingilie entry yako katika sehem ya control price ukiingilia hapo unaweza ukapigwa kwanza kisha Soko likaenda upande wako* 😆😆😆

BADA YAKUZIJUA HIZO LEO TUISHIA HAPO TUTAENDELEA TENA MBE WAKATI UJAO

Niwakumbushe tu yakwamba bado tunaendelea namasomo katika darasa ya FBI MASTER CLASS  vitu hivyo tunavionesha kwa vitendo nakuingia huko unaingia kwa ghalama ya 20000TSH tu kwa ofa ya mwisho wa mwaka badala ya 40000TSH iliyozoeleka wahi ukasome na ukaanze mwaka mpya kwakishindo

.........................................by...............................................................................................

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

ads

ads