BASICS OFFOREX (PATTERNS FORMATION) PART FOUR

                                                      REVERSAL PATTERN

Hizi ni Chart Pattern zenye Kuonesha Uwezekano Mkubwa Wa Kugeuka Kwa Soko. Mfano Soko Lilikua Uptrend Alaf Ukaona Reversal Pattern Kweny Kilele cha Uptrend Ujue Soko Linageuka Kua DownTrend. 

Soko Hua Lina Change From Ongoing Trend au Old Trend To New Trend Kwa Kutoa Reversal Pattern, Haliwezi Kugeuka Kiholela Holela Tu.


                                    Zifuatazo Ni Reversal Pattern:


1. M au W Pattern.

M Pattern Hua Inafahamika kwa Jina La *Double Tops*


W Pattern Hua Inafahamika Kwa Jina La *Double Bottom*

2. Triple Top and Triple Bottom

3. Head And Shoulders.


4. Wedges (Rising and Falling)

Hizi Reversal Pattern Hutokea Pale Ambapo Soko Lilikua Strong kwa Upande Mmoja, Mfano Uptrend Alaf likawa Limekua Exhausted (Lime-Overbuy) hivyo Linatakiwa Kubadili Uelekeo.

Triple Bottom Ni Kinyume Cha Triple Top

                                                   Tuanze na M pattern


👉Hii ni structural pattern ambayo inakua formed pale ambapo Soko linakua lilitokea chini na kwenda Juu kuishia katika ukingo wa resistance 


👉huwa na viambata vifuatavyo ,1. Top Mbili Juu 2. neckline 


👉huwa tunaitumia ikiwa ipo Juu ya market structural Nyingine zote na Nje na hapo inakua ni trap


👉Angalia mfano hapo chini

*Hayo Maelezo hapo Juu yanakua yanafanana na yanakua kinyume chake na pattern ya W*

Hapa maana yake market inakua ilikua inashuka hivyo Basi inageuza uelekeo kwakukupatia W ambapo Ndani yake inakua na double bottom na inaambatana na uwepo wa neckline 

Note neckline ikivunjwa inakua retested au inakua retested kabla haijavunjwa🙏

                                                 

Hapa hii ni clear M ambapo inakua imeshatengeneza top Mbili km inavyooneka hapa mshare no 1 na no 2 ambapo ukiangalia katika hizo top Mbili utakutana na reversal candlestick nilizofundisha pale Juu, utakutana Kila top either INA engulfing candlesticks au twizzer au morning star au doji au hammer na nyinginezo ukikutana na hii  utakutana na Eneo linaloitwa neckline nimeoneshwa na mshare no 3 hapo ndo wengi huwa wanapigika😆 Kule ju wameshakupatia reversal double top yaan clear M lkn hapo kwenye neckline wanawezakukupatia reversal candlestick zitakazokuonesha yakua market itabuy ili uingie mtegoni nakuhalibu psychology yako (psychomotor with market behavior) ukiwa unaelewa ukufanyacho unakua unapiga Soko pamoja na dealer😆😆


Bila shaka mnaona hapo namna pattern Yetu ilivyokaa vzr na entry yake inatakiwa iwe katika Mguu wa pili wa W ,


                                                                  Angalizo👇

Hapo unaweza ukatoka ktk TF Kubwa ukakutana na market imetengeneza twizer formation candlestick tu with no m or w formation hivyo inatakiwa ushuke TF ndogo ambapo utakutana na clear m au w

                                                     Then tuangalie Tripple top na Tripple bottom

Hapa market huwa inakua katika zone either kwenye resistance (supply) au kwenye support (demand) ambapo inaikalia mala tatu hiyo zone


Mfano👇👇👇👇





Hapo nadhani tunakua tunaelewana vizr ambo hii inakua very strong structural pattern , hapa unakua na Faida nyingi endapo tyr unajua Vitu hivi👉Aina ya candlestick 👉iliyotengenezwa hiyo candlestick👉zone uliyopo 😆😆😆hapa usipokua makini unajipiga mwenyewe badala ya kupigwa na broker😆


*Sifa za Tripple top zinakua zinafanana na Tripple bottom kama nilivyooneshwa hapo juu*

Hapa ukiitambua market ilipo kazi inakua imebakia kumuua broker tu

                                                              Note

To every reversal pattern there is a reversal candlestick*🙏🙏


                                                                   Head and shoulders


 *Hii ni structural pattern ambayo ipo katika mvumo wa bega la kushoto kisha kichwa na kumalizia na bega la kulia*

👉hii pia hutuonesha yakua dealers are to change the direction of the market

Hapa ina kupasa uwe na inner eye na ili uwe na inner eye lazima ujue Kuunganisha matukia at once 

👉mtambue adui kabla hajakutambua

👉muue adui kabla hajakuua

😆😆😆

Wengi huchelewa kuona ndy maana wanaonwa kwanza wao kisha wanauawa


1👉bega la kushoto 👉2 .kichwa👉3. Bega la Kulia    hapa maana yake ilitakiwa market uikute kwenye bega la Kulia kisha  uisell na hapo lazima ukutane na candlestick reversal zinazokuonesha usell🙏


*Kinyume chake unakutana na inverted head and shoulders itakayokua ni structural pattern yakubuy* 🙏
*Ya mwisho mhim tuone wedges (rising and falling)*

Hapa lazima tujua yakua market Yetu huwa ni wave like motion (inatembea katika mfumo wa mawimbi) mfano👇👇👇👇


Hapo Bila shaka mnoaona nilivyovionyesha ambapo hii market ilikua inapanda Juu hivyo waves zakushuka zitakua ndogo na waves zakupanda zitakua Kubwa nadhani tulizungumzia trends za market katika some lililopita hivyo katika hizo waves tutakutana  na reversal candlestick au utakutana na reversal pattern humo ambapo inakua imeform kitu kiitwacho pattern within pattern na strong inayoendesha market ni ile iliyotengenezwa kwenye bottom au at a top of the market😁

Flag na Wedges Hua Zinafanana Sana Na Usipoweza Kuzitofautisha Huwez Jua Kipi Ni Kipi, But Mambo Yapo Waz Kabsa Kama Ifuatavyo:

1. FLAG 👉 hizi zinakua Na Upper Resistance Line na  Lower Support Line. Hii Mistari Hua Ipo Sambamba, Haiwez Kutana. Kwahio Unapochora Flag Yako Ni lazima Uhakikishe Mistari Yako Inayotumika Kama Limits (Upper na Lower) Inakua Sambamba.


2. Wedges 👉 Hii Inakua Na Upper Resistance Line na Lower Support Line, Ila Mistari Yake Inakwenda Inapungua, Kitaalamu Tunaita Price Constriction Au Shrinking , Hivyo Mistari yake Inakwenda Ikiwa Inapunguza Pips Range za Resistance na Support line, Price Itakwenda Ikiwa Inapungua na Ikifika Mbele Sana Zinaweza Kukutana. Baada Ya Price Kufanya Constriction Mwisho Wa Wedge Ina Burst (Fumuka) na Kufanya Strong Move.









Triangle Nazo Zipo Za Aina Mbili, Ascending na Descending. Ascending inakua Na Horizontal Upper Resistance Line, Na Chini Inakua Na Support ilikaa Katika Mfumo Wa Kupanda, Means Buyers Wanaongeza Nguvu, Mwisho Wa Siku Wanaivunja Hio Upper Resistance Line na Soko Linapanda. Descending Triangle inakua Na Horizonatal Lower Support Line, na Kwa Juu inakua Na Resistance iliokaa Katika Mfumo Wa Kushuka, Na Hivyo Inaonesha Nguvu ya Sellers Kua inaongezeka Mwishowe Inatoboa Hapo Kweny Support line Na Kushuka Chini.




Pennant ni Isometric Triangle. Nazo Zipo Mbili Ya Bullish Na Bearish, hivi Zitategemea Na Move Inaelekea Wapi. Hii pattern Mim Hua Siipendelei.


NDUGU ZANGU BILA SHAKA MMEELEWA VIZURI KUHUSIANA NA PATTERN NA MATUMIZI YAKE SASA TUKUTANE PART 5 KWENYE ZONE



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

ads

ads