Acha tuendelee na somo letu na tutaendelea na trend tofauti na pattern kama nilivyowaahidi kwenye part two hii nikwamba nahitaji upate mtililiko mzuri ambao hautakusumbua katika kuelewa mambo
TRENDS
Tunapozungumzia trend tunazungumziea uelekeo wa soko ambapo soko lina uelekeo wa juu, chini au pembeni hivyo tunaweza weka aina za trend kuwa tatu lakini katika website hii nitakuelezea aina nne za trend kwa kina na kwa undani zaidi ili upate kuelewa namna unawezalichambua soko nakukuletea pesa inayokusitahili kuliko kuipoteza hela yako kwakuyafanya mambo yasiyositahili
Tuna Aina nne na za market trend ambapo wengi wameziozoea tatu ambazo ni;
👉 tuna upward trend
👉Downward trend
👉Sideway (horizontal trend)
Wengi wamezizoea hizo tu na wamekua wakiipa Majina sawa na;
👉 Raging market (chopping market)
Ambayo hii ni ya nne na tutaona utofauti wake katika Maelezo hapo chini.
Tuanze na Upward trend
👉Hii inaonesha uelekeo wa Juu wa market ambapo market inakua inatokea chini kwenda katika upande wa Juu.
👉 katika uelekeo huu wa market huwa inatutengenezea swing high high na swing high low
Mfano ni huu hapa ambapo ;HH👉ni High high ,na HL👉 ni HL mda mwingine HH huwa wanaita peak formation high na Hl mda mwingine wanaita peak formation low ,pia Majina ni mengi na wengine huita swing high au swing low
Hapa huwa tunatafuta specific entry katika sehem Maalum ,ikiwa tupo kwenye upward trend huwa tunafanya entry kwenye hizo Hl na high low ya kwanza inakua nzuri Zaidi kuingia Sokoni hiyo ni kwakupunguza risk ,na hapo TP huwa tunaichukulia katika HH located area
Down trend
👉Hii ni Aina ya trend ambapo market huwa inatembea kwa kutengeneza low low na low high
👉Ikiwa inamaanisha market inashuka chini km mfano unavyoonekana hapa chini
Mfano ni huu hapa na hapa entry nzr huwa tunaingia ktk LH ambapo unakua umeipungunza risk kabisa
Na hizo Mbili yaani down trend na uptrend zinakua tamu mno kufanya entry but ukichemka entry bora ulambe pilipili 😆😆
Tuje Aina ya tatu sideway (horizontal trend)
👉Hii ni Aina ya trend ambayo mda mwingine wanaiita ranging market .
👉 Huwa inakua na organised pips kutoka Juu na chini
👉 hii pia huwa inatengeneza High high na low low tu
Aina ya nne ambayo tunaiita choppigi market,
👉hii ni Aina ya market ambayo inakosa mwelekeo Maalum ambapo kunakua na ugum wa kuzitambua peak za high high au low low
👉 market hii mpangilio wake unakua wa hovyo usioeleweka
👉market hii huwa tunasema uachane Nayo usiingie Sokoni kabisa
Market ya namna hii huwa ni market ya hovyo mno na huwa inapoteza mda mwingi mpaka ubongo unauma ,unakua unaingia kwenye blue Mara red😆😆😆masaa kama kumi unakua hupati chcht hapa Mdomo hukauka mno😆 lkn ukitambua haisumbui
mpka hapo umeshaelewa maana ya hizo trend na ninaimani umeelewa maana na namna yakuzitumia hizi trend
NOTE; unapokutana na uptrend soko huwa linazivunja HH na huwa linaziheshimu HL na ikivunja hizo HL ni dalili tosha yakua unaweza ukawa umeshaanza kupewa trend mpya, na vivyo hivyo unapokutana na down trend huwa inazivunja LL na huzitunza LH na zikivunjwa basi tayari wanakua wanakupatia viashilia vikubwa kukwambia kwamba unabadilishiwa trend
angalia mwonekano wa hizi chart hapa chini;
Kama uonavyo chart hapo juu ambayo ni down trend hivyo inakuonesha kabisa yakua LL ndizo zilizokua zinavunjwa soko likiwa linashuka chini na tunaona LH zikiwa zinatunzwa soko likifika huko linaziheshimu na hazifunjwi na hivyo kuwa na vigezo vyote vilivyotimia kuwa down trend
Sasa ndungu msomaji nawe nikuachie kazi moja tengeneza uptrend na uielezee vizuri nione kama hili somo umelielewa vizuri na kwa kina
Kipengele kijacho ni pattern formation , namna maumbo mbalimbali yanavyotengenevyo kwenye biashara ya forex na matumizi yake usikose maana nimhim ninaimani utaelewa vyema maana ni somo ambalo limeshiba vizuri
............MWISHO KATIKA PART THREE TUKUTANE PART FOUR...........
Post a Comment