BASICS OF FOREX PART TWO (CANDLESTICS REFORMS WITH ITS INFORMATION)

 CANDLESTICK PATTERNS & PSYCHOLOGY BEHIND THEIR FORMATION

Hapa Tunajifunza Aina Mbali mbali za Candlestick Pattern Na Kwann Vipo Hivyo. 

Kuna Candlestick Pattern  nying ila Zipo za Umuhimu, Kama Ifuatavyo.

Candlestick Pattern inaweza Kua Ni Muunganiko Wa Candlestick zaidi ya Moja Au Hata Candle Moja Inatosha Kutoa Clear Pattetn Yenye Kuleta Maana Inayoeleweka Sokoni.

           ACHA TUANZE NA MOJA BAADA YA NYINGINE;

                                                1. DOJI PATTERN

Hii ni Aina Ya Pattern Ambayo inahusisha Candlestick Moja Tu Tena Isiyokua Na *Real Body* 

Doji Huonesha InDecision Kati ya Sellers na Buyers (Yani ukiona Hii Pattern Ujue Hakuna Alietawala Soko) Sababu Open Price Na Close Price Zinakua Sehemu Moja, Hazina Ile Body yenye Kuonesha Nani AmeControl Soko. Kwahio Kwenye Doji Huwez Jua Nani Amelitawala Soko Kwa Muda Huo.

Kwenye Hii Doji Kuna Neutral Na Long Tailed Doji.

Neutral Inaonesha Urefu Sawa Kwa Kila Mstari, I Mean High, Low, Open And Close Price Vipimo Vyao Vinakua Na Urefu Sawa. 

Long Tailed Doji Ni Doji Yenye Tail/Shadow/Wick Ndefu


                                        2. Grave Stone Doji.

Hii ni Doji Iliokaa Kama Msalaba Wa Kiisalam (Yale Mawe Yao Wanayowekaga Kaburin) 

Tail ya Chini Inakua Ndogo au Hamna Kabsa Lakin Juu inakua Na Long Tail.

Tafsiri Yake ni Kwamba, Soko Lilikua Na Nguvu ya Kupanda Juu (Ndio Maana Tuna Long Upper Tail Lakin Sellers Waliingia Mchezon na Kuishusha Thaman Chini)

                                          3. Kinyume Cha Grave Stone Doji Ni *Dragonfly*

Maelezo Yote Yafanye Kinyume Utapata Maelezo Ya DragonFly

Indecision Kati ya Buyers Na Sellers

Kwahio Kama Muda Unatoka Kushoto Kwenda Kulia, Soko Nalo litakua Linatoka Kushoto Kuelekea Kulia.




                                                                     
Hizo ndizo aina za Doji candlestics  na na matumizi yake

                                         

                                                                          PIN BAR PARTTERN 

PIN BAR PATTERN hii ni Pattern ya Candlestick Moja yenye Tail/Wick Ndefu Na Body Ndogo Sana. Ndio Maana Ikaitwa Pin Bar, inafanana Na Pin. Pin Bar Zipo Za Aina Mbili, Bearish Pin Bar Ambapo kichwa Kinakua Chini (Rangi Haimati Sana Hapa Lengo ni Saikoloji ya Kuundwa Kwake). Bullish Pin Bar Kichwa Kinakua Juu, Rangi Haina Madhara.

                                                      


ANGALIA PICHA NYINGINE HAPA CHINI ZIKIWA N MANA HIYO HIYO

                                                                    


Psychology ya Bullish Pin Bar, Ni Kwamba Sellers Walilivuta Soko Mpaka Ulipoishia Mkia Huko Chini, ila Buyer Wakaja Na Nguvu Kubwa Wakalirudisha Soko Juu Ndio Maana Ina Mkia Mrefu Chini Alaf Body Ndogo.





                                                                             


Psychology ya Bearish Pin Bar, Ni Kwamba Buyers Walilivuta Soko Mpaka Ulipoishia Mkia Huko Juu, ila Sellers Wakaja Na Nguvu Kubwa Wakalirudisha Soko Chini, Ndio Maana Ina Mkia Mrefu Juu, Alaf Body Ndogo.



                                                                 HARAMI

Harami Candlestick Pattern Hii ni Pattern Yenye Candleatick Mbili, Ya Kwanza inakua Kushoto Alaf Inakua Kubwa na Ya Pili Inakua Kulia Alaf Inakua Ndogo. Maana Ya Neno Harami Ni Ujauzito Au Mimba. Kwahio Kendo Kubwa Inachukuliwa Kama Mama, Alaf Kendo Ndogo Inachukuliwa kama Ujauzito (Mtoto). Tuna Harami Za Aina Mbili. 1 👉 Bullish Harami, hii inatokea Kwenye Downtrend ambapo inatakiwa akubadilisha Soko Kua Uptrend, Bullish Haram, Inakua Na Kendo Kubwa Ya Kusell ikifatiwa Na Kendo Ndogo ya Kubuy


                                                                   



Bearish Harami, Inatokea Kwenye Uptrend, na Lengo ni Kuifanya Uptrend Kua Downtrend. Mother Candle Inakua Bullish ikifatiwa Na Mtoto (Ujauzito) unaokua Bearish.

Ona mfano halisi hapa chini na namna iwezavyo kukupatia tarifa ya nini kitatokea

                                                                      


na bullish harami huoneka ka picha ilivyo hapo chini kikubwa ujue key levels , na hapa watu wanajiuliza key level ni kitu gani au kinafananaje usiwaze wala usihofu tutanyumbulisha vitu vyote katika hii blog ka nayo karibu utaelewa , angalia hii bullish harami hapa chini

                                                                          

bila shaka unashuhudia kinachoendelea hapo katika hiyo chart juu sasa angalia hii ya hapa chini kinachotokea

                                                                    
Tuangalie aina nyingine ya candlestic hapa chini (morning na evening stary)

                                                          

MORNING STAR hii ni pattern yenye kendo 3, ya Kwanza inakua Bearish, ya Pil Bullish yenye Body ndogo, ikifatiwa Na Bullish Kubwa, Kama Unavyoona Hapo. Hii pattern inatokea Kwenye Downtrend ili kulibadili soko kua Uptrend. Kwahio ukiiona Hio Ujue Soko linapanda Unatakiwa Ubuy


                                                                    

EVENING STAR hii ni pattern yenye kendo 3, ya Kwanza inakua Bullish, ya Pil Bearish yenye Body ndogo, ikifatiwa Na Bearish Kubwa, Kama Unavyoona Hapo. Hii pattern inatokea Kwenye Uptrend ili kulibadili soko kua Downtrend. Kwahio ukiiona Hio Ujue Soko litashuka, Unatakiwa Usell


                                                                        TWEEZER FORMATION

Hizo Ni Candlestick Pacha, Zinakua Mbili Zenye Kufanana Size (Body na Wick Zake pia), ila Utofauti Wao Ni kwamba Moja Inakua Bullish Na Nyingne Inakua Bearish. Kuna Aina Mbili za Tweezer Pattern Aina Hizi inategemea na Candlestick Gani Imeanza Kwenye hio Pattern na Imetokea Eneo Gan La Trend

                                                                                 

Wakati Mwingne Tweezer Zinaitwa Rail Way Track Au Rail Road Track (RRT)

AINA ZA TWEEZER.

1.Tweezer Bottom

2. Tweezer Top

Angalia Ufanano wa Size Zao, Usikariri Umbo, Mana Nyingne Unaweza Kuta Hazina Umbo la Hivyo ila Zikawa Ni Mapacha



Tweezer Botton inatokea Kwenye Downtrend, kaz yake ni Kubadili Soko Kutoka Downtrend Kuwa Uptrend, Hivyo Ukiziona Hizo Unatakaiwa Kubuy. Tweezer Top Zinatokea Kweny Uptrend, kaz yake ni Kubadil Soko Kua Downtrend Hivyo Ukiziona Hizo Unatakiwa Kusell.






                                                     
Marubozu Candlestick Ni Candlestick Zenye Kuonesha Momentum kubwa Ya Soko kuelekea Upande Fulan yaweza Kua Chini iwapo Marubozu ni ya kusell na yaweza Kua Juu iwapo Marubozu ni ya Kubuy. Tafsiri nzuri ni kusema Kwamba Stock imenunuliwa Kwa Nguvu kubwa Kwa Uekekeo Mmoja. Marubozu Zinaweza Zisiwe na Wicks/tail kabsa na kama Zitakua na Tail basi ni Ndogo Sanaaa  na Kama Zitakua na Wick/Tail bas Open na Close Price, Zinakua Karibu Sana na High na Low Za Tail (hii ni kuonesha Kua Hakukua na mvutano kat ya Buyers na Seller) yan mmoja Tu ndo Alikontroo soko kwa Nguvu zote.

Marubozu Hua Ni ishara Kubwa Sana Ya Big Players (BIG BOYS) Kuingia Sokoni, Mara Nying Hua Zinatokea Mwanzoni mwa Trend Mpya. Ukiona Marubozu Candlestick mwanzon mwa Trend (Hasa Ukitumia Tf kubwa mfano Daily) Basi Jua kua Utakua Na Strong Trending Market.


Kwa Sifa Hio, Marubozu Ikapewa Jina La TREND BAR au TREND CANDLESTICK




Trend Bar Hatuzitumii Popote Tu maana Danganya Toto(Fake Out) ni Nying Sana Sokoni, hivyo Kuna Maeneo Muhimu ya Kutumia Trend Bar, Maeneo yenyewe Ndio Hayo mawili Tuliyoyaona.


Lazima utambue trend ya trade yako na kisha uzitumie zinazoenda kwenye upande wa trend yako ,,,.....,trend ni uelekeo wa Soko ambao wawezakua wa Juu au chini km nilivyoelekeza Kule mwanzo


Reality na mahali zinapotokea huonesha clear direction ya market baada yakutoka ktk mfumo wa consolidation ama wakati wa kubadili trend


Maana yake ndo kigezo nilichotumia kusell hapo na mpaka Sasa Nipo kwa profit



M pattern Ni Hio Hapo, lkn ukipanda kwenye 4H utakutana na ile pattern yetu


Market ilkua Inapanda, ila Ikafika Hapo Kweny Zone Alaf Ikatengeneza Trend Bar Kweny H4. Ukishuka H1 unakuta Sifa Kama Hizo, LH, LL & LH. Hizo sifa Zinatuambia Kwamba Soko Linashuka, Ndio Maana Nikasell hapo.

Kwahio Kikubwa Ni Kujua:

1. Maana Ya Marubozu

2. Itokee Wapi ili iwe Profitable

3. Inatumikaje (Mara Nging Hua Inakua Retested Mpaka Nusu Yake)

4. Saikoloj ya Marubozu Hasa Kweny Tf Kubwa Ina Tuambia Nn Sokon.

Mwandishi *SUN TZU* Anasema *Kujijua Wewe Ni Sehemu Ya Vita, ila Kumjua Adui Yako Itakufanya Ushinde Zaidi*

Sasa Tumeshajua Namna Ya Kuitumia Marubozu(Kujijua). Je Ni Wakati Gani Hatutakiwi Kuitumia ? (Kumjua Adui)

Kwan hutokea mda wote trend inapoanzaa au baadh ya muda tuu na je retresment yake n lazma iwe nusu na je retresment icpotokea je

Niliulzwa Swali la hivi huko,,,,majibu👇👇👇

Mara Nying Trend Bar Hua Zinatokea Mwanzon Mwa Trend, na Hii ndio Inayotupatia Momentum Gaining, Kwa Lugha Nying Naiitaga Momentum Gaining Candlestick (MGC).

Retracement yake Mara Nying Huishia Nusu Ya Marubozu (ila Hii Usikariri Maana Mbelen Tutakua Na Course ya PULLBACK full Package Itaeleza Kila Kitu Juu ya Retecement)

Naongezea Maelezo Kwenye aya Ya Kwanza.

Kunapokua Na Trend Change ni Lazima Kuwe na Vitu Viwili.

1. Old trend 👉 hii inakua Imeshatambea Muda Mrefu na Inakua Imeishiwa Nguvu hivyo Ni lazima Kuwe na *Momentum Decrease*, Hii tunaiona Kwa Kuangalia Candlestick Zake, Zinakua Ndogo Ndogo Sana na Zinakua Zinacheza Eneo Moja Ili Zitafute Namna Ya Kubadilika. 

2. New Trend 👉 Baada Ya Momentum Loss/Decrease Kweny Old Trend, Ni Lazima Tupate Momentum Gaining Candlestick (Marubozu) ili Kufanya Trend Change,  Mana Bila HivyoTrend Haibadiliki. 

Kwahio Ni Vyema Kujua Hio Concept Vzuri ili Uwe Makin Sokon

                                


Hapo tunamwambao wa Aina Mbili ambapo kuanzia no 1 tunaona trade Yetu inatokea kubadili mwelekeo na kuanza kupanda with high momentum ilipofika no Mbili inapunguza momentum na kutupatia structure ya kuchuka  M' pattern na baada ya hapo inatupatia trade bar iliyooneshwa na no 3 (nilionesha pale Juu na extended chart) na baada ya hapo tunaona trade inaanza kushuka kufuata direction iliyooneshwa na no 4 with high momentum

                                                             

Candlestick Range au Price Range* 👉Hii ni Distance kutoka Kweny Top ya Upper Shadow/Wick na Bottom ya Lower Shadow/Wick. Kwa Lugha Rahisi Ni Urefu Wa Candlestick Kutoka Chini Mpaka Juu.


                                 UMUHIMU WA CANDLESTICK RANGE

Candlestick Range ni Muhimu Katika Kugundua *Volatility* ya Stock (Currency pair).

Ninaposema *Volatility*  Namaanisha *Speed ya Pair Kwa Muda Husika* ukiona Candlestick Range ni Kubwa Ujue Pair Hio Ni Volatile kwa Muda Huo na Ukiona Candlestick Range ni Ndogo Ujue Volatility ni Ndogo. 

Speed ikiwa Kubwa Candlestick Range Inakua Kubwa (Inabeba Eneo Kubwa) 

Speed ikiwa Ndogo Candlestick Range inakua Ndogo Pia.


Pia unaweza Ukaangalia Volatility ya Pair Mbali Mbali Kwa Kuangalia Speed Zao, Yani Kwa Candlestick 1 Soko linakua Limetembea Pips Ngapi.



*INSIDE BAR CANDLESTICK PATTERN* 👉 Hii ni Pattern Inayohusisha Candlestick mbili, Candle Ya Kwanza Inakua Kubwa Alaf Candle ya Pili Inakua Ndani Ya Candlestick Range Ya Previous Candle (Candle ya Nyuma/Kwanza)

Inside Bar Candlestick Pattern Inafanana Sana Na Harami, ila Tu Hii Inside Bar Candle Ya Pili (Ndogo) Hua Ipo Ndani Ya Candlestick Range Ya Candlestick Kubwa (Ya Nyuma). Kwa Upande Wa Harami Candle Ndogo inaweza Kutoka Nje Kidogo Ya Candlestick kubwa (Mother Candleatick)

Matumizi Ya INSIDE BAR*

Kwanza Kabsa Inabidi Ufahamu Kwann Inside Bar Imeundwa Hivyo (Psychology Behind Its Formation)

Kwenye Inside Bar Patten Tuna Candlestick Mbili, Mother Candle (Candle kubwa) na Inside Bar yenyew (Mtoto). Formation Hii Inatuambia Kua Soko Halikufanya Move Ya Kuendelea Na Uelekeo Wa Mother candle, Hivyo CandleStick Ndogo (Inside) Tunaichukulia Kama *PullBack/Consolidation* au Ishara Ya Kubadilika Kwa Trend iwapo Trend itakua Kweny Kikwazo Kikubwa (Key Levels) ambapo Yaweza Kua Ni *Strong Support au Resistance

Kwahio Kama Inside Bar Yaweza Kua *Pullback au Reversal Sign* Tunatakiwa Kusubiri Hio Inside Bar Ivunjwe, Yani Tusubiri Candlestick Inayofata Baada Ya Inside Bar ili Tuone Imefungaje, Imeivunja/Imeipita Inside Bar Kwa Chini Au Kwa Juu Then Tutapata Uelekeo wa Soko Kwa Kuangali Inside Bar imevunjwa Kwa Upande Gani. Mara Nying Tunapata Maamuzi Baada ya Momentum Gaining Candlestick (MGC) kuivunja Inside Bar au Kukiwa Na Candlestick Yenye Kuonesha Strong Rejection mfano PIN BAR CANDLESTICK.

                                           

Inside Bar Ikifatuwa na Pin Bar (Strong Rejection ya Price Kwenda chini)

Tunaposema Candlestick Tunagusa Vitu Muhim Vifuatavyo:

1. Body

2. Open price

3. Close price

4. Upper Wick

5. Lower Wick

6. High price

7. Low price.

Hivyo Nikikwambia Inside Candlestick Inatakiwa Kuwa Ndani Ya Previous Candlestick Range, Means Vitu Vyote vya Inside Bar Candlestick Vinatakiwa kua Ndani Ya Previous Candlestick Range

                                       

Mpaka hapo ndugu zangu ninaimani mmeelewa vizuri sana kuhusiana na maswala ya cancdlestic maana yake na matumizi yake na namna ziwezavyo kukupatia faida sokoni , kuna watu wanatengeneza pesa ndefu kwakutumia tu elimu hii ya candlestic ninachokusihi jifunze fanya mazoezi utafanikiwa


kinachofuata ni PATTERNS NA MANA YAKE NA NAMNA YAKUZITUMIA

....................................MWISHO WA PART TWO KITAKACHO FUATA NI PART THREE........



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

ads

ads